19 Septemba 2025 - 18:34
Juhudi zinaendelea kuiadhibu Israel katika michezo kutokana na vita yake dhidi sya Gaza

Wakati mbio kubwa za baiskeli nchini Hispania zilikumbwa na vurugu za waandamanaji waliopinga ushiriki wa timu ya Israel, mataifa kadhaa ya Ulaya yametishia kususia tukio maarufu la burudani endapo Israel itaruhusiwa kushiriki.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wakati mbio kubwa za baiskeli nchini Hispania (Vuelta a España) zilikumbwa na maandamano dhidi ya timu ya Israel, mataifa kadhaa ya Ulaya sasa yanatishia kususia tukio kubwa la burudani iwapo Israel itashiriki.

Wimbi la upinzani wa kimataifa dhidi ya utawala wa Israel kutokana na athari kubwa za kibinadamu za vita vya Gaza limevuka mipaka ya siasa, na sasa linaonekana wazi katika medani za michezo na utamaduni. Wakosoaji wa Israel wanasema kuwa haifai kuruhusiwa kushiriki katika matukio ya kimataifa wakati inadaiwa kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina.

Mashinikizo yakiongezeka, lakini taasisi kuu za michezo bado hazijachukua hatua

Hadi sasa, Israel bado haijafungiwa rasmi na mashirika makubwa ya kimataifa ya michezo kama vile Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) au FIFA (Shirikisho la Soka la Dunia). Licha ya hayo, mashirika madogo kama Shirikisho la Kimataifa la Muay Thai limeonesha nia ya kuchukua hatua. Kwa ujumla, dunia ya michezo imekuwa na uvuguvugu mkubwa katika kuchukua msimamo dhidi ya Israel.

Waziri Mkuu wa Hispania awaunga mkono waandamanaji

Waziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sánchez, alichochea mjadala zaidi wiki hii kwa kuunga mkono waandamanaji wa Kipalestina waliovuruga mbio hizo, akisema kuwa: “Ni wakati wa kuisusia Israel kwenye matukio ya kimataifa ya michezo hadi ukatili wa Gaza utakapoisha.”

Eurovision pia yatikiswa

Siku moja baada ya matamshi ya Sánchez, runinga ya taifa ya Hispania iliungana na nchi nyingine tatu za Ulaya kutishia kujiondoa kwenye mashindano ya Eurovision ya mwaka ujao ikiwa Israel itaruhusiwa kushiriki. (Kwa mujibu wa Associated Press)

Hollywood nayo yatoa tamko

Mapema mwezi huu, baadhi ya watayarishaji filamu wa Hollywood, waigizaji na watu mashuhuri katika tasnia ya burudani walitia saini azimio la kususia taasisi za filamu za Israel, zikiwemo maonesho ya filamu, vituo vya runinga na kampuni za uzalishaji.

FIFA yazidi kunyamaza

FIFA, ambayo imekuwa ikikumbana na malalamiko rasmi kutoka kwa Shirikisho la Soka la Palestina, ilikataa kutoa maoni kuhusu sera yake dhidi ya Israel au maendeleo ya uchunguzi wa malalamiko hayo. Palestina imekuwa ikidai kwa muda mrefu kwamba Israel inakiuka haki za wachezaji na vilabu vya Palestina, na imeomba ifungiwe kushiriki mashindano ya FIFA.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha